Habari
MMUYA APOKEA TAARIFA ZA TATHMINI YA MPANGO KABAMBE WA JIJI LA DODOMA NA MIKAKATI YA UPANGAJI MATUMIZI YA ARDHI
- 29 Sep, 2026
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Kaspar Mmuya (MB), amepokea Taarifa ya Tathmini ya Utekelezaji wa Mpango Kabambe wa Jiji la Dodoma wa mwaka 2019–2039, iliyowasilishwa na wataalamu wa Maendeleo ya Makazi kutoka Makao Makuu kwa kushirikiana na Ofisi ya Kamishna Msaidizi wa Ardhi Mkoa pamoja na Halmashauri ya Jiji la Dodoma.
Sambamba na hilo, Mhe. Mmuya amepokea pia taarifa kutoka kwa wataalamu wa Tume ya Taifa ya Mipango ya Matumizi ya Ardhi (NLUPC) kuhusu mikakati ya Tume katika upangaji, usimamizi na utekelezaji wa Mipango ya Matumizi ya Ardhi kupitia fedha za Miradi ya Maendeleo katika mwaka wa fedha 2026/2027.
Taarifa hizo zimewasilishwa leo, Septemba 29, 2026, katika Ofisi za Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mtumba, Jijini Dodoma.