Habari

WAZIRI NDEJEMBI KUFANYA ZIARA ENEO LA KURASINI

  • 09 Jan, 2025
WAZIRI NDEJEMBI KUFANYA ZIARA ENEO LA KURASINI

WAZIRI wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Deogratius Ndejembi amefanya kikao cha pamoja na wawakilishi wa wananchi 41 ambao hawakupokea fidia katika eneo lililopo Kurasini wilayani Temeke, Dar es Salaam lililotwaliwa na kulipwa fidia Mwaka 2008 na kumilikishwa kwa Muwekezaji wa Kampuni ya Tanzania Road Haulage.

Mhe. Waziri Ndejembi ameahidi kufanya ziara katika eneo hilo mara moja ili kupata ufumbuzi wa mgogoro huo ulioudumu kwa miaka 17.

Kikao hicho kimefanyika Januari 04, 2025 katika Ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Mhe. Sixtus Mapunda, Wataalamu kutoka Wizarani na Mwakilishi wa Kampuni ya Tanzania Road Haulage.