Habari

MAWAZIRI NDEJEMBI, BASHUNGWA ZIARANI KOREA KUSINI

  • 09 Sep, 2024
MAWAZIRI NDEJEMBI, BASHUNGWA ZIARANI KOREA KUSINI

WAZIRI wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Deogratius Ndejembi na Waziri wa Ujenzi, Mhe. Innocent Bashungwa pamoja na Maafisa wa Wizara hizo Septemba 07, 2024 wamewasili jiji la Seoul nchini Korea Kusini na kupokelewa na Balozi wa Tanzania nchini Korea Kusini, Mhe. Togolani Mavura kwa ziara ya kikazi.

 

Mawaziri hao wamefanya ziara hiyo kwa mwaliko wa Waziri wa Ardhi, Ujenzi na Uchukuzi wa Jamhuri ya Korea, Mhe. Sangwoo Park ambapo pamoja na mambo mengine watashiriki Mkutano wa Kimataifa wa Ushirikiano wa Miundombinu kati ya Afrika na Jamhuri ya Korea (Global Infastructure Cooperation Conference - GICC 2024)

 

 Aidha, katika ziara hiyo Mawaziri watapata fursa ya kukuza ushirikiano na taasisi ya Fedha ya Korea kwa ajili ya Ujenzi (K - FINCO) mnamo mwezi Julai, 2024 walifanya ziara nchini Tanzania wakiongozwa na Dkt. Lee Eun Jae, ambapo walisaini hati za Makubaliano (MoUs) kati ya K-FINCO na TANROADS pamoja na NHC na TBA.