Habari

MAELEKEZO YA WAZIRI MKUU YAZIDI KUTEKELEZWA DODOMA

  • 22 May, 2026
MAELEKEZO YA WAZIRI MKUU YAZIDI KUTEKELEZWA DODOMA

Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Kaspar Mmuya, ameendelea kusikiliza na kutatua kero za ardhi za wananchi kutoka maeneo mbalimbali ya Jiji la Dodoma.

 

Zoezi hilo limefanyika leo, Alhamisi, Mei 21, 2026, ambapo Mhe. Mmuya amekutana na wananchi hao katika Ukumbi va Halmashauri ya Jiji la Dodoma kwa ajili ya kupokea na kuzitafutia ufumbuzi changamoto zao.

 

Hatua hiyo ni mwendelezo wa utekelezaji wa maelekezo ya Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba yanayomtaka kila kiongozi kushuka chini na kushughulikia kikamilifu migogoro ya ardhi nchini ili kuwaletea wananchi haki na maendeleo.

 

Ikumbukwe kuwa Mei 20, 2026 wakati akisikiliza na kushughulikia kero za wananchi wa maeneo ya Mahomanyika, Ndachi, Mbuyuni na Nkuhungu Broad Acres katika kikao kilichofanyika katika Ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma alimuelekeza Naibu Waziri Kaspar Mmuya kusikiliza hoja za wananchi hao.