Habari
KLINIKI YA ARDHI YASOGEZA HUDUMA ZA ARDHI KWA WANANCHI MBARALI
- 16 Oct, 2025

Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi inaendesha zoezi la Kliniki za Ardhi katika maeneo mbalimbali hapa nchini ili kusogeza huduma za ardhi karibu na wananchi katika maeneo yao.
Akizungumza na wananchi wa Kata ya Igurusi wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Bi. Lucy Kabyemera amesema katika mwezi Oktoba 2025 timu ya wataalamu kutoka wizara hiyo inaendelea kutoa huduma za Kliniki za Ardhi katika mikoa ya Arusha, Mbeya, Mtwara, Njombe, Pwani na Tabora.
“Zoezi hili ni utekelezaji wa maelekezo ya Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan aliyoyatoa kwa Wizara kusogeza karibu huduma za ardhi kwa wananchi, tuna ofisi Ardhi zakatika mikoa yote 26. Tumeenda mbele zaidi kwa kutoka kwenye ofisi zetu na kuwafuata wananchi na kutoa huduma za sekta ya Ardhi” amesema Naibu Katibu Mkuu Bi. Lucy.
Aidha, Wizara hiyo inatekeleza falsafa ya 4R za Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ikiwemo uboreshaji wa mifumo ya utendaji kazi wa utoaji huduma ambapo sasa hivi wizara inatumia mfumo wa e-Ardhi ambao unatumika kutoa huduma za masuala ya ardhi.
Mwitikio wa wananchi wa Halmashauri ya Mbarali KATIKA kata za Igurusi. Ubaruku na Rujewa ni takriban 557 wamefika na wamepata huduma katika zoezi la Kliniki za Ardhi linaloendelea wilayani humo.