Habari
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii yakagua miradi ya NHC
- 19 Oct, 2026
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii, ikiongozwa na Mwenyekiti wake, Mhe. Timotheo Mzava (Mb), imekagua maendeleo ya ujenzi wa miradi mitatu ya nyumba inayotekelezwa na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) jijini Dodoma.
Ziara hiyo imefanyika Oktoba 19, 2026, ambapo wajumbe wa Kamati walitembelea miradi mbalimbali, ikiwemo mradi wa Madeli wenye thamani ya Shilingi bilioni 41, mradi wa Iyumbu wenye thamani ya Shilingi bilioni 18.5 na mradi wa Njedengwa wenye thamani ya Shilingi bilioni 58.09.
Wajumbe wa Kamati walipata fursa ya kukagua ubora wa kazi zinazofanyika, kujionea hatua zilizofikiwa katika ujenzi na kutathmini utekelezaji wa miradi hiyo kwa kuzingatia mipango na viwango vilivyowekwa.
Katika ziara hiyo, Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Kaspar Mmuya aliambatana na Katibu Mkuu Mhandisi Anthony Sanga, wajumbe wa Menejimenti ya Wizara pamoja na Menejimenti ya Shirika la Nyumba la Taifa wakiongozwa na Mkurugenzi Mkuu wake Bw. Hamad Abdallah.