Habari

KAMATI YA BUNGE YAPOKEA TAARIFA YA UTEKELEZAJI BAJETI YA WIZARA YA ARDHI KWA NUSU MWAKA 2024/2025

  • 24 Jan, 2025
KAMATI YA BUNGE YAPOKEA TAARIFA YA UTEKELEZAJI BAJETI YA WIZARA YA ARDHI KWA NUSU MWAKA 2024/2025

Kamati ya Kudumu ya Ardhi, Maliasili na Utalii chini ya Mwenyekiti wake Mhe. Timotheo Mzava Januari 23 2025 imepokea na kujadili taarifa ya utekelezaji wa Bajeti ya Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kipindi cha nusu mwaka kuanzia Julai hadi Desemba 2024.

Katika kikao hicho, Kamati hiyo ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii ilipokea pia taarifa ya utekelezaji wa Bajeti ya Tume ya Taifa ya Mipango ya Matumizi ya Ardhi.

Wizara imeshiriki vikao Kamati hiyo kuanzia Januari 20 hadi 23, 2025 kuhudhuriwa na Viongozi wa Wizara wakiongozwa na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Deogratius Ndejembi, Naibu wake Mhe. Geophrey Pinda, Katibu Mkuu Mhandisi Anthony Sanga, Naibu Katibu Mkuu Lucy Kabyemera, wajumbe wa Menejimenti ya Wizara pamoja na Wakuu wa taasisi ambazo zipo chini ya wizara za Shirika la Nyumba la Taifa na Tume ya Taifa ya Mipango ya Matumizi ya Ardhi.