Habari

KAMATI YA BUNGE YAENDELEA KUJADILI TAARIFA ZA WIZARA YA ARDHI

  • 17 Oct, 2024
KAMATI YA BUNGE YAENDELEA KUJADILI TAARIFA ZA WIZARA YA ARDHI

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi , Maliasili na Utalii imeendelea kujadili taarifa za Wizara ya Ardhi ambapo imepokea na kujadili taarifa ya Utendaji wa Tume ya Taifa ya Mipango ya Matumizi ya Ardhi pamoja na Utendaji wa Ofisi ya Msajili wa Hati.

 

Wasilisho la taarifa hizo limefanyika leo tarehe 16 Oktoba 2024 ambapo Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Geophrey Pinda aliwaeleza wajumbe wa Kamati hiyo mikakati ya namna wizara yake inavyofanya jitihada za kuiboresha sekta nzima ya ardhi nchini.

 

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi Maliasili na Utalii chini ya Mwenyekiti wake Mhe. Timotheo Mzava inaendelea na vikao vyake vya kupokea na kujadili taarifa za wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi kabla ya kuanza kwa vikao vya Bunge siku ya jumanne tarehe 29 Oktoba 2024