Habari

HATI ZA KIMILA: MKOMBOZI WA WANANCHI WA MELELA NA MIKESE MKOANI MOROGORO

  • 31 Aug, 2026
HATI ZA KIMILA: MKOMBOZI WA WANANCHI WA MELELA NA MIKESE MKOANI MOROGORO

Wananchi wa Vijiji vya Melela na Mikese mkoani Morogoro wameeleza furaha yao baada ya kupata Hati za Kimila, hatua inayowawezesha kutambuliwa kisheria na kuimarisha usalama wa umiliki wa ardhi.

 

Akizungumza katika mahojiano maalumu yaliyofanyika Agosti 28, 2026, katika Banda la Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi lililopo Uwanja wa Jamhuri mkoani Morogoro, Mwenyekiti wa Kijiji cha Mikese Mjini, Kata ya Mikese, Bw. Mohammed Kalungwana, pamoja na Bw. Alfred Mudugwa kutoka Kijiji cha Melela, wamesema Hati za Kimila ni mkombozi kwa wananchi, kwani zinawapa uhakika wa umiliki wa ardhi na kuwawezesha kutumia ardhi yao kama nyenzo ya kiuchumi.

 

Wamesema kuwa hati hizo pia zinawawezesha wananchi kuomba mikopo katika taasisi za fedha, kupunguza migogoro ya ardhi na kuongeza thamani ya ardhi, hivyo kuchochea maendeleo ya familia na jamii kwa ujumla.

 

Hati ya Kimila – Ulinzi wa Ardhi, Amani na Maendeleo.