Habari
HATI MILKI ZA ARDHI 107,683 ZAANDALIWA NA KUSAJILIWA
- 04 Jun, 2026
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Dkt. Leonard Akwilapo amesema Wizara ya yake imefanikiwa kuandaa na kusajili hati milki za ardhi 107,683 hadi kufikia Mei 2026.
Mhe. Dkt. Akwilapo amesema hayo Mei 28, 2026 wakati akiwasilisha Bajeti ya Wizara kwa mwaka wa fedha 2026/2027 Bungeni jijini Dodoma.
Amesema, katika kipindi hicho Wizara pia imeandaa na kusajili Hati za Hakimiliki ya Kimila 99,762, Vyeti vya Ardhi ya Kijiji 148, na Hati za Sehemu ya Jengo 914.
Aidha, ameweka wazi kuwa, jumla ya Miamala ya Hatimiliki na Nyaraka za Kisheria 137,681 zimesajiliwa sawa na asilimia 137.68 ya lengo.
Ametoa wito kwa wananchi kuhakikisha wanamiliki ardhi zao kisheria ili kuepuka migogoro na kuwawezesha kutumia ardhi kwa ajili ya kujiletea maendeleo ya kiuchumi na kijamii.