Habari

BUNGE LAPITISHA ZAIDI YA BILIONI 169.6 WIZARA YA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI

  • 28 May, 2024
BUNGE LAPITISHA ZAIDI YA BILIONI 169.6 WIZARA YA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI

Bunge limepitisha Bajeti ya Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kiasi cha Sh. 169,628,415,000/= kwa kishindo ili kutekeleza majukumu yake ya sekta ya Ardhi kwa mwaka wa Fedha 2024/2025.

 

Wabunge wakiongozwa na Mhe. Kassim Majaliwa, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wamewapongeza Mhe. Jerry Silaa, Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi pamoja na Naibu Waziri wake Mhe. Geophrey Pinda kwa kazi nzuri ya kuwahudumia Watanzania kwenye sekta ya Ardhi nchini.

 

Pongezi hizo zimetolewa na Wabunge mara baada ya kuhitimishwa kwa shughuli za Bunge na Mhe. Dkt. Tulia Mwansasu Mei 27, Bungeni jijini Bodoma.