Habari

ARDHI FC YAIANZA SHIMIWI KWA USHINDI WA BAO 1-0 DHIDI YA RAS LINDI

  • 23 Sep, 2026
ARDHI FC YAIANZA SHIMIWI KWA USHINDI WA BAO 1-0 DHIDI YA RAS LINDI

Timu ya mpira wa miguu ya Wizara ya Ardhi, Nyunba na Maendeleo ya Makazi (Ardhi  Fc) imeanza vyema Mashindano ya Shirikisho la Michezo ya Wizara na Idara za Serikali (SHIMIWI) baada ya kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Ras Lindi katika mchezo  wa kwanza wa hatua ya makundi.

Mchezo huo umechezwa Septemba 23, 2026, katika Uwanja wa Shule ya Msingi Mweleni mkoani Kilimanjaro ulikuwa wa ushindani mkubwa, huku timu zote zikionyesha juhudi na ari ya kutafuta matokeo.

Hata hivyo, Ardhi FC ilifanikiwa kutumia vyema nafasi iliyopata na kufunga bao moja lililoamua mchezo huo, na hivyo kuondoka na pointi tatu muhimu katika hatua hiyo ya makundi.

Ushindi huo unaipa Ardhi FC mwanzo mzuri katika safari yake ya mashindano hayo, huku ikitarajiwa kuendelea kupambana katika michezo inayofuata ya hatua ya makundi.

Mashindano ya SHIMIWI yanaendelea  Mkoani Kilimanjaro, yakishirikisha timu kutoka Wizara na Idara mbalimbali za Serikali.