Taarifa Muhimu

UTOAJI WA HUDUMA NYAKATI ZA USIKU KATIKA OFISI ZA ARDHI MKOA WA DAR ES SALAAM

Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi anapenda kuwajulisha wananchi wa Mkoa wa Dar es Salaam kuwa, tarehe 22 — 26 Oktoba, 2024 Ofisi za Ardhi Mkoa pamoja na Halmashauri zote za Mkoa wa Dar es Salaam zitatoa huduma kwa wananchi kuanzia saa 1.30 asubuhi hadi wakati wa usiku.