Taarifa Muhimu

UTAMBUZI WA MAWAKALA WA MILKI (REAL ESTATE AGENTS AND BROKERS)

Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi inaratibu na kuendesha zoezi la kutambua kampuni zote zinazojihusisha na shughuli za Uwakala wa Milki/watu binafsi katika uuzaji/upangishaji wa nyumba/viwanja na mashamba. Hatua hii inalenga kuboresha utoaji wa huduma za sekta ya Milki nchini.