Taarifa Muhimu

UHUISHAJI WA VYETI VYA UDALALI WA BARAZA LA ARDHI NA NYUMBA LA WILAYA

Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi inapenda kuwakumbusha Madalali wa Baraza wenye nia ya kuomba kuhuisha vyeti vyao kuwasilisilisha maombi yao kwa mujibu wa Kanuni ya 13 ya Kanuni za Uteuzi, Malipo na Nidhamu ya Madalali na Wasambaza Nyaraka.

Maombi ya kuhuisha Vyeti yawasilishwe kupitia Fomu Maalum (Fomu Na. 6) ya Kanuni za Uteuzi, Malipo na Nidhamu kwa Madalali wa Baraza na Wasambaza Nyaraka (Tangazo la Serikali Na. 172 la 2023).