Taarifa Muhimu

UFAFANUZI KUHUSU NOTISI YA KUSUDIO LA KUTWAA ARDHI CHINI YA FUNGU LA 6 LA SHERIA YA UTWAAJI ARDHI (SURA 118)

Kupitia Gazeti la Serikali Toleo namba 550 la tarehe 29 Novemba 2024 ilitolewa Notisi kwa Umma kuwa ardhi yenye ukubwa wa mita za mraba 233,000 zilizopo Manispaa ya Ubungo na Kinondoni kwenye maeneo yaliyopo katika makutano ya barabara ya Bagamoyo na Kunduchi Mbuyuni (mita za mraba 156,000); makutano ya Sam Nujoma na Chuo Kikuu cha Ardhi Mkabala na Mlimani City (mita za mraba 24,000); eneo lililopo Manispaa ya Ubungo Simu 2000 (mita za mraba 35,000); na Boko Basiaya (mita za mraba 18,000) kuwa inakusudiwa kutwaliwa kwa matumizi ya umma. Maeneo hayo yatahusisha ujenzi wa karakana kuu, maegesho ya magari na vituo vya mrishi.