Taarifa Muhimu
TANGAZO KWA UMMA KUHUSU RASIMU YA MPANGO WA UENDELEZAJI UPYA ENEO LA SINZA 2026 - 2046
- 27 Mar, 2026
- Pakua
Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi imepokea rasimu ya Mpango wa Uendelezaji Upya eneo la Sinza kutoka Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo. Kwa mujibu wa kifungu cha 14 (1) cha Sheria ya Mipangomiji Sura 355 Toleo la mwaka 2023, Mkurugenzi wa Mipangomiji anawatangazia wananchi na wadau wa maendeleo wa Manispaa ya Ubungo kuwa amepokea Rasimu ya Mpango wa Uendelezaji Upya eneo la Sinza 2026-2046.