Taarifa Muhimu

MPANGO WA UENDELEZAJI UPYA ENEO LA SINZA (SINZA REDEVELOPMENT PLAN 2026 - 2046)

Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kushirikiana na Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo zinaandaa mpango wa uendelezaji upya (Redevelopment Plan) ambao utaongeza uthibiti na usimamizi wa uendelezaji wa miundombinu ya ujenzi ikiwemo ujenzi shadidi (Vertical development) unaoendelea kutokana na kasi ya ukuaji pamoja na uhitaji mkubwa wa ardhi kwa ajili ya shughuli za kijamii na kiuchumi katika eneo la Sinza.