Kurasa

Kitengo cha Mawasiliano Serikalini

Majukumu ya Kitengo cha Mawasiliano Serikalini ni pamoja na: -

i. Kuandaa na kusambaza nyaraka mbalimbali kama vile vipeperushi, makala, jarida (newsletters) na nyenzo nyingine za mawasiliano kwa lengo la kuuelimisha Umma kuhusu sera, programu, shughuli na mageuzi yanayotekelezwa na Wizara;

ii. Kuratibu maandalizi na uendeshaji wa mikutano na taarifa kwa vyombo vya habari ya Wizara;

iii. Kushiriki katika mazungumzo na mawasiliano na Umma pamoja na vyombo vya habari kuhusu masuala yanayohusu Wizara;

iv. Kuelimisha na kuhamasisha Umma kuhusu shughuli, programu na sera za Wizara;

v. Kuratibu maandalizi ya nyaraka za kisekta na za Wizara kwa ajili ya warsha, makongamano na mikutano mbalimbali;

vi. Kuratibu uandishi na uchapishaji wa makala za Wizara katika magazeti; Kusasisha taarifa za kisekta na za Wizara katika tovuti ya Wizara; na

vii. Kushauri Idara, Vitengo, Taasisi zilizo chini ya Wizara pamoja na Taasisi za Umma zisizo za kibiashara kuhusu uandaaji na uzalishaji wa nyaraka mbalimbali.