Habari
WIZARA YA ARDHI YASHIRIKI UZINDUZI WA DIRA 2050 JIJINI DODOMA
- 18 Jul, 2025

Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhandisi Anthony Sanga ameshiriki kwenye hafla ya uzinduzi wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 iliyofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete (JKCC),jijini Dodoma tarehe 17 Julai, 2025.
Akizungumza baada ya Uzinduzi wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 Mhandisi Sanga amesema Dira hiyo ni shirikishi kwa kuwa imeshirikisha makundi mbalimbali.
Kuhusu Sekta ya Ardhi kwenye Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025, Mhandisi Sanga amesema kuwa Sekta ya Ardhi imehusishwa hasa eneo la usimamizi madhubuti wa Ardhi kwa kuhakikisha kila kipande cha ardhi kinatambulika.
Pamoja na mambo mengine, matarajio ya Dira hii ni kuwa na nchi iliyopangwa vizuri na kuweka wazi matumizi ya ardhi yakiwemo ya makazi, kilimo, mifugo, viwanda na hifadhi.