Habari

WAZIRI MKUU AKABIDHI HATI KWENYE MAONESHO

  • 24 Jun, 2024
WAZIRI MKUU AKABIDHI HATI KWENYE MAONESHO

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa (Mb.) amekabidhi hati za kumiliki ardhi kwa wananchi waliotembelea banda la Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwenye Maonesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma katika viwanja vya Chinangali jijini Dodoma leo tarehe 23 Juni 2024. 

 

Mhe. Waziri Mkuu amekabidhi hati hizo kwa wananchi wakati alipotembelea mabanda ya maonesho kwenye kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yaliyozinduliwa tarehe 16 Juni 2024 na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. George Simbachawene (Mb.).