Habari

WAKURUGENZI WA HALMASHAURI KATIKA WILAYA ZA MKOA WA TABORA WAAGIZWA KUTENGA FEDHA KWA AJILI YA SEKTA YA ARDHI

  • 07 Mar, 2024
WAKURUGENZI WA HALMASHAURI KATIKA WILAYA ZA MKOA WA TABORA WAAGIZWA  KUTENGA FEDHA KWA AJILI YA SEKTA YA ARDHI

Mkuu wa Mkoa wa Tabora Balozi Dkt. Batilda Burian amewaagiza Wakurugenzi wa Halmashauri katika Wilaya za mkoa huo kutenga fedha kwa ajili ya sekta ya ardhi katika Bajeti ya mwaka 2024/25 ili kuendeleza utekelezaji katika maeneo yale ambayo Mradi wa Uboreshaji Usalama wa Milki za Ardhi (LTIP) hautekelezwi.

 

Mkuu wa mkoa huo Balozi Dkt. Batilda amesema wadau wa ardhi mkoa wa Tabora watumie fursa ya wamejadili namna ya kutekeleza Mradi wa Uboreshaji Usalama wa Milki za Ardhi (LTIP) katika mkoa huo wakiongozwa na kaulimbiu inayosema ‘‘Usawa Wa Kijinsia Katika Umiliki Wa Ardhi Kwa Ustawi Wa Jamii Yetu’’

 

Akifungua mkutano huo Machi 6, 2024 mkoani Tabora, Mkuu wa mkoa huo Balozi Dkt. Batilda Burian amesema wadau hao waepata muda mwafaka wa kujadili mwelekeo wa jinsi mradi utakavyotekelezwa na kujadiliana namna bora ya kutatua changamoto zitakazojitokeza klatika halmashauri zao.

 

“Mkutano huu umekuja muda muafaka katika mkoa wetu hasa mwezi huu wa Machi ambao unaenda sanjari na Siku ya Wanawake Duniani yanayoongozwa na kaulimbiu inayosema ‘‘Wekeza kwa Wanawake Kuharakisha Maendeleo ya Taifa na Ustawi wa Jamii’’ ni ni heshima kubwa mradi huu kutekeleza katika Wilaya zetu” amesema Balozi Dkt. Batilda.

 

Mradi huo unatekelezwa katika mkoa wa Tabora katika halmashauri za Kaliua, Sikonge, Uyui, Urambo, Nzega Mjini, Nzega Vijijini na Manispaa ya Tabora.

 

Mkuu wa Mkoa amesisitizitiza kuwa Mkoa huo upo mstari wa mbele katika kutekeleza mradi wa Uboreshaji wa Usalama wa Milki za Ardhi kwa maendeleo ya wananchin wa Mkoa huo. 

 

Aidha, Mkuu wa Mkoa  amesataka watalaam wa sekta ya ardhi washirikiane na viongozi wa Serikali za mitaa na vijiji kuwapa wananchi elimu kuhusu masuala ya ardhi ili kutoa taarifa sahihi ambazo zitasaidia kurahisisha utekelezaji wa mradi huo.

 

Kwa upande wake Mratibu wa Mradi wa LTIP Bw. Joseph Shewiyo amesema mradi huo unanalenga kupanga matumizi ya ardhi kwa maendeleo ya vijiji na miji, kuhamasisha umiliki wa ardhi kwa pamoja, kuzingatia haki za makundi maalum katika umiliki wa ardhi pamoja na usawa wa kijinsia.