Habari
TUMIENI ARDHI NDANI YA MIPAKA YENU - NAIBU WAZIRI KASPAR MMUYA
- 20 Dec, 2025
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Kaspar Mmuya amewataka wananchi kutumia ardhi kwa kuheshimu alama za mipaka zilizowekwa Kisheria wakati wanatekeleza shughuli zao za maendeleo
Mhe. Kaspar ametoa kauli hiyo leo Desemba 17,2025 katika kijiji cha Nanjilanje kilichopo wilayani Ruangwa mkoani Lindi wakati mkutano wa hadhara kwa ajili ya kukabidhi hati miliki za ardhi kwa wananchi wa kijiji hicho.
Amesema thamani ya shughuli za maendeleo katika jamii zitagemea amani na Utulivu hivyo kusheshumu matumizi ya Ardhi na mipaka ilyopo kwenye ramani ya kiwanja au shamba husika kutaondoa migogoro ya mipaka.
"Tumia shughuli zako za maendeleo kwenye mipaka ya kwako". amesema Naibu Waziri Mmuya
Mheshimiwa Naibu Waziri amewasisitiza wananchi wa Nanjilanje kuwa wanayo dhamana kubwa ya kuilinda hatimiliki kwani ina faida kubwa ikiwamo kutumika kama dhamana ya kuombea Mikopo katika taasisi za kifedha .
"Hati hii kwako ni dhamana ya rasilimali uliyopewa, kwa hiyo unawajibu wa kuona thamani ya kipande cha Ardhi unayopewa leo". amesema Naibu Waziri Mmuya
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Ruangwa Mheshimiwa Hassan Ngoma ameishukuru Serikali ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kupitia Wizara ya Ardhi kwa kuwezesha zoezi upimaji na Urasimishaji wa vijiji 50 ikiwemo Nanjilanje ndani ya Miaka Minne.
"Tunampongeza na Kumshukuru sana Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ndani ya miaka minne amefanya upimaji na Urasimishaji kwa vijiji zaidi ya 50" amesema Hassan Ngoma Mkuu wa Wilaya ya Ruagwa.
Aidha Mheshimiwa Ngoma amemuomba Naibu Waziri Mmuya kusaidia kupatikana kwa Suluhu ya kudumu ya migogoro ya Mipaka kati ya Vijiji vya Mtondo, Mkaranga na Nambilanje.
Jumla ya hatimiliki za kimila 2161 zimeandaliwa na kupitia mpango wa matumizi bora ya Ardhi chini ya Tume ya Matamizi ya Ardhi ya Taifa kwa kushirikiana na Ofisi ya Kamishna msaidizi wa Ardhi Mkoa wa Lindi na halmashauri ya Ruangwa katika vijiji vya Nambilanje na Mkatila.