Habari
SERIKALI KUPUNGUZA GHARAMA ZA VIFAA VYA UJENZI
- 14 Nov, 2025
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amesema, serikali itapunguza gharama za Vifaa vya Ujenzi ili kuwawezesha wananchi kujenga Makazi Bora.
Serikali pia itaweka mkazo maalumu kwenye Nyumba bora na nafuu, kusimamia utekelezaji wa Sera zinazolenga kuboresha hali ya makazi kwenye maeneo yenye makazi duni.
Akizungumza wakati wa ufunguzi rasmi wa Bunge la 13 tarehe 14 Novemba 2025 jijini Dodoma, Mhe Dkt Samia ameongeza kwa kusema, serikali itashirikiana na sekta binafsi ili kuongeza uwekezaji kwenye miradi ya uendeleza Miji kwa kujielekeza kwenye ujenzi wa Nyumba za bei na nafuu yaani Affordable House.
Aidha, amesema, serikali itaimarisha utatuzi wa migogoro ya ardhi kwa kupima ardhi nchi nzima kwa kutumia teknolojia ya kisasa ya satelite sambamba na kuongeza kasi ya urasimishaji maeneo ya makazi nchini.